Waamuzi 2:4
Malaika wa Bwana alipomaliza kusema mambo haya kwa Waisraeli wote, watu wakalia kwa sauti kuu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
5Wakapaita mahali pale Bokimu. Nao wakamtolea Bwana sadaka. 1 Kifo Cha Yoshua
Cross References
1 Samuel 7:6Walipokwisha kukutanika huko Mispa, walichota maji na kuyamimina mbele za Bwana. Siku hiyo walifunga na wakaungama, wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi ya Bwana.” Naye Samweli alikuwa kiongozi + 7:6 Kiongozi hapa maana yake mwamuzi. wa Israeli huko Mispa.
Ezra 10:1Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana.
Jeremiah 31:9Watakuja wakilia; 2 wataomba wakati ninawarudisha. 1 Nitawaongoza kando ya vijito vya maji 2 katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa, 1 kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, 2 naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza. 1
Zechariah 12:10“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema + 12:10 Au: Roho wa neema. na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.
Luke 7:38Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Yesu akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.
James 4:9Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni.