Waamuzi 4:2
Hivyo Bwana akawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Jemadari wa jeshi lake alikuwa Sisera, aliyeishi huko Haroshethi-Hagoyimu + 4:2 Haroshethi-Hagoyimu ina maana Haroshethi ya Mataifa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
1Baada ya Ehudi kufa, Waisraeli wakafanya tena maovu machoni pa Bwana.
Cross References
Joshua 11:10Wakati huo Yoshua akarudi na kuuteka mji wa Hazori na kumuua mfalme wake kwa upanga. (Hazori ulikuwa mji mkuu wa falme hizo zote.)
Judges 2:14Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
Judges 4:16Lakini Baraka akafuata magari pamoja na jeshi mpaka Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia.
1 Samuel 12:9“Lakini wakamsahau Bwana Mungu wao, hivyo Mungu akawauza katika mkono wa Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori na katika mikono ya Wafilisti na mfalme wa Moabu, ambaye alipigana dhidi yao.
Isaiah 50:1Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako 2 ambayo kwayo niliachana naye? 1 Au nimewauza ninyi kwa nani 2 miongoni mwa watu wanaonidai? 1 Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, 2 kwa sababu ya makosa, mama yenu aliachwa. 1