Walawi 18:25
Hata nchi ilitiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake, nayo nchi ikawatapika wakazi wake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 18:28Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia.
Numbers 35:33“ ‘Msiinajisi nchi mnayoishi. Umwagaji damu hunajisi nchi, na upatanisho hauwezekani kufanyika katika nchi ambayo damu imemwagwa, isipokuwa tu kwa damu ya yule aliyeimwaga damu.
Deuteronomy 9:5Si kwa sababu ya haki yenu wala uadilifu wenu kwamba mtaimiliki nchi yao; lakini kwa sababu ya uovu wa mataifa haya, Bwana Mungu wenu atawafukuza mbele yenu, ili kutimiza lile alilowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo.
Ezra 9:11uliyoyatoa kupitia watumishi wako manabii uliposema: ‘Nchi mnayoiingia kuimiliki ni nchi iliyochafuliwa na uovu wa watu wake. Kwa matendo yao ya machukizo wameijaza nchi kwa unajisi wao kutoka mwisho mmoja hadi mwingine.
Psalms 106:38Walimwaga damu isiyo na hatia, 2 damu za wana wao na binti zao, 1 ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, 2 nayo nchi ikanajisika kwa damu zao. 1
Isaiah 26:21Tazama, Bwana anakuja kutoka makao yake 2 ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao. 1 Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake, 2 wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.