Leviticus 19:16
“ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako. “ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
17“ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.
Cross References
Exodus 20:16Usimshuhudie jirani yako uongo. 1
Exodus 23:7Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia.
1 Kings 21:10Lakini waketisheni watu wawili wabaya kabisa mkabala naye, nao washuhudie kuwa yeye amemlaani Mungu na mfalme. Kisha mtoeni nje na kumpiga kwa mawe hadi afe.”
Psalms 50:20Wanena daima dhidi ya ndugu yako 2 na kumsingizia mwana wa mama yako. 1
Proverbs 10:18Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, 2 na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu. 1
Proverbs 20:19Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika, 2 kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi. 1