Leviticus 2:14
“ ‘Kama ukileta malimbuko ya sadaka ya nafaka kwa Bwana, utatoa masuke yaliyopondwa ya nafaka mpya iliyookwa kwa moto.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15Weka mafuta na uvumba juu yake; ni sadaka ya nafaka.
Cross References
Genesis 4:3Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana.
Leviticus 23:10“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi nitakayowapa na kuvuna mazao ya nchi hiyo, leteni kwa kuhani mganda wa nafaka ya kwanza mtakayovuna.
Leviticus 23:14Kamwe msile mkate wowote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, mpaka siku ile mtakayomletea Mungu wenu sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi. 1 Sikukuu Ya Majuma (Hesabu 28:26-31)
Numbers 28:2“Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’
2 Kings 4:42Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutokana na nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Elisha akasema, “Wape watu ili wale.”
Isaiah 53:2Alikua mbele yake kama mche mwororo 2 na kama mzizi katika nchi kavu. 1 Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake, 2 hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani. 1