Leviticus 27:28
“ ‘Lakini chochote kile mtu alicho nacho na akakiweka wakfu + 27:28 Akakiweka wakfu ina maana ya kumpa Mungu kabisa, daima, bila kurudiwa. kwa Bwana, iwe ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, hakiwezi kuuzwa au kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
29“ ‘Mtu yeyote aliyewekwa wakfu ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe.
Cross References
Exodus 22:20“Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa Bwana, lazima aangamizwe.
Leviticus 27:21Shamba hilo litakapoachiwa mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwa Bwana, nalo litakuwa mali ya makuhani.
Numbers 21:2Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwa Bwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.”
Deuteronomy 13:15kwa hakika ni lazima mwaue kwa upanga wale wote wanaoishi katika mji ule. Uharibuni kabisa, pamoja na watu wake na mifugo yake.
Deuteronomy 25:19Bwana Mungu wako atakapokupa pumziko mbali na adui zako wote wanaokuzunguka katika nchi akupayo kuimiliki kuwa urithi, utafutilia mbali kumbukumbu lote la Waamaleki chini ya mbingu. Usisahau!
Joshua 6:26Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Aliyelaaniwa mbele za Bwana ni mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko: 1 “Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume 2 ataiweka misingi yake; 1 kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho 2 atayaweka malango yake.”