Luke 1:20
Basi sasa kwa kuwa hujaamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati wake, utakuwa bubu hadi siku ile mambo haya yatakapotukia.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
21Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zekaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni.
Cross References
Exodus 4:11Bwana akamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu kuona au upofu? Je, si mimi, Bwana?
2 Kings 7:2Yule afisa ambaye mfalme alikuwa anauegemea mkono wake akamwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama Bwana atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Elisha akajibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!” 1 Mwisho Wa Kuzingirwa
Isaiah 7:9Kichwa cha Efraimu ni Samaria, 2 na kichwa cha Samaria 2 ni mwana wa Remalia peke yake. 1 Kama hamtasimama thabiti katika imani yenu, 2 hamtaimarika kamwe.’ ”
Ezekiel 24:27Katika siku ile kinywa chako kitamfumbukia yeye aliyenusurika, nawe utaongea wala hutanyamaza tena. Hivyo wewe utakuwa ishara kwao, nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.”
Mark 16:14Baadaye Yesu akawatokea wale wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa wakila chakula. Akawakemea kwa kutoamini kwao na kwa ugumu wa mioyo yao kwa kutosadiki wale waliomwona baada yake kufufuka.
Luke 1:45Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.” 1 Wimbo Wa Maria Wa Sifa