Luke 13:8
“Yule mtunza shamba akamjibu, ‘Bwana, uache tena kwa mwaka mmoja zaidi, nami nitaupalilia na kuuwekea mbolea.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 32:11Lakini Mose akamsihi Bwana Mungu wake, akasema, “Ee Bwana, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu?
Exodus 34:9Mose akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.” 1 Kufanya Agano Upya (Kutoka 23:14-19; Kumbukumbu 7:1-5; 16:1-17)
Joshua 7:7Yoshua akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, kwa nini umewavusha watu hawa ngʼambo ya Yordani ili kututia mikononi mwa Waamori watuangamize? Laiti tungeliridhika kukaa ngʼambo ile nyingine ya Yordani!
Jeremiah 14:7Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu, 2 Ee Bwana, tenda jambo kwa ajili ya jina lako. 1 Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa, 2 nasi tumetenda dhambi dhidi yako. 1
Jeremiah 15:1Kisha Bwana akaniambia: “Hata kama Mose na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende!
Joel 2:17Makuhani, ambao wanahudumu mbele za Bwana, 2 na walie katikati ya ukumbi 2 wa Hekalu na madhabahu. 1 Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee Bwana. 2 Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa, 2 neno la dhihaka kati ya mataifa. 1 Kwa nini wasemezane miongoni mwao, 2 ‘Yuko wapi Mungu wao?’ ” 1 Jibu La Bwana 1