Luke 6:8
Lakini Yesu alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Inuka usimame mbele ya watu wote.” Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Chronicles 28:9“Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana Bwana huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele.
Job 42:2“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, 2 wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika. 1
Isaiah 42:4hatazimia roho wala kukata tamaa, 1 mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia. 2 Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.” 1
Mark 3:3Yesu akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.”
Luke 13:12Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.”
John 9:4Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.