Luke 8:42
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Yesu alipokuwa akienda, umati wa watu ukamsonga sana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 44:20Nasi tukakujibu, ‘Tunaye baba yetu ambaye ni mzee; pia yupo mwanawe mdogo aliyezaliwa katika uzee wake. Ndugu yake amekufa, na huyu mdogo ndiye mwana pekee kwa mama yake aliyebaki, naye baba yake anampenda.’
Job 4:20Kati ya mawio na machweo 2 huvunjwa vipande vipande; 1 bila yeyote kutambua, 2 huangamia milele. 1
Psalms 103:15Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, 2 anachanua kama ua la shambani; 1
Ezekiel 24:16“Mwanadamu, kwa pigo moja nakaribia kukuondolea kile kilicho furaha ya macho yako. Lakini usiomboleze au kulia wala kudondosha machozi yoyote.
Zechariah 12:10“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema + 12:10 Au: Roho wa neema. na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.
Luke 7:12Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mwanamke.