Luke 8:43
Katika umati huo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu, wala hakuna yeyote aliyeweza kumponya.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 16:12Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa Bwana bali kwa matabibu tu.
Psalms 108:12Tuletee msaada dhidi ya adui, 2 kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. 1
Isaiah 55:1“Njooni, ninyi nyote wenye kiu, 2 njooni kwenye maji; 1 nanyi ambao hamna fedha, 2 njooni, nunueni na mle! 1 Njooni, nunueni divai na maziwa 2 bila fedha na bila gharama. 1
Mark 5:25Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili.
Mark 9:21Yesu akamuuliza baba yake, “Mwanao amekuwa katika hali hii tangu lini?” Akamjibu, “Tangu utoto wake.
Luke 13:11Wakati huo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na minane, wala alikuwa hawezi kunyooka wima.