Malachi 1:2
Bwana asema, “Nimewapenda ninyi.” “Lakini ninyi mnauliza, ‘Wewe umetupendaje?’ ” Bwana asema, “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
1Ujumbe: Neno la Bwana kwa Israeli kupitia kwa Malaki. 1 Yakobo Alipendwa, Esau Alichukiwa
Cross References
Genesis 25:23Bwana akamjibu, 1 “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, 2 na mataifa hayo mawili 2 kutoka ndani yako watatenganishwa. 1 Mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine, 2 na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”
Genesis 25:26Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo. + 25:26 Yakobo maana yake Ashikaye kisigino, au Atwaaye mahali pa mwingine, au Mdanganyaji, au Mwenye hila, au Mlaghai, au Mjanja. Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa.
Genesis 27:33Isaki akatetemeka kwa nguvu sana, akasema, “Alikuwa nani basi, ambaye aliwinda mawindo akaniletea? Nilikula kabla tu hujaja na nikambariki, naye hakika atabarikiwa!”
Genesis 28:13Juu yake alisimama Bwana, akasema, “Mimi ni Bwana, Mungu wa baba yako Abrahamu na Mungu wa Isaki. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.
Genesis 48:4naye akaniambia, ‘Nitakufanya ustawi na kuongezeka hesabu yako, nitakufanya kuwa jamii ya mataifa, nami nitakupa nchi hii uimiliki milele wewe na wazao wako baada yako.’
Deuteronomy 7:6Kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wako. Bwana Mungu wako amekuchagua wewe kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia kuwa watu wake, hazina yake ya thamani.