Mark 10:51
Yesu akamuuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
50Akiwa analivua lile joho lake, alisimama na kumwendea Yesu.
52Yesu akamwambia, “Nenda zako, imani yako imekuponya.” Mara akapata kuona, akamfuata Yesu njiani.
Cross References
2 Chronicles 1:7Usiku ule Mungu akamtokea Solomoni na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.”
Matthew 7:7“Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.
Mark 10:36Naye akawaambia, “Je, mwataka niwafanyie jambo gani?”
John 20:16Yesu akamwita, “Maria!” Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu).
Philippians 4:6Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.