Mark 11:18
Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria wakapata habari hizi, nao wakaanza kutafuta njia ya kumuua, kwa kuwa walikuwa wakimwogopa, kwa sababu umati wote ulikuwa unashangazwa na mafundisho yake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
19Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji. 1 Mtini Ulionyauka (Mathayo 21:20-22)
Cross References
1 Kings 18:17Ahabu alipomwona Eliya, akamwambia, “Je, ni wewe, mtaabishaji wa Israeli?”
1 Kings 22:8Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumuuliza shauri la Bwana, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.” Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”
Isaiah 49:7Hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye Mkombozi na Aliye Mtakatifu wa Israeli, 1 kwake yeye aliyedharauliwa na kuchukiwa na taifa, 2 kwa mtumishi wa watawala: 1 “Wafalme watakuona na kusimama, 2 wakuu wataona na kuanguka kifudifudi, 1 kwa sababu ya Bwana, aliye mwaminifu, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, aliyekuchagua wewe.” 1 Kurejezwa Kwa Israeli
Matthew 21:15Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika.
Matthew 21:45Viongozi wa Makuhani na Mafarisayo waliposikia mifano ya Yesu, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao.
Mark 1:22Watu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana aliwafundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wa sheria.