Mark 13:8
Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na mitetemeko sehemu mbalimbali na njaa. Haya yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 15:6Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina.
Isaiah 19:2“Nitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri, 2 ndugu atapigana dhidi ya ndugu, 2 jirani dhidi ya jirani, 2 mji dhidi ya mji, 2 ufalme dhidi ya ufalme. 1
Jeremiah 4:31Nasikia kilio kama cha mwanamke 2 katika utungu wa kuzaa, 1 kilio cha uchungu kama cha anayemzaa 2 mtoto wake wa kwanza: 1 kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua, 2 akiinua mikono yake, akisema, 1 “Ole wangu! Ninazimia; 2 maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”
Jeremiah 13:21Utasema nini Bwana atakapowaweka juu yako 2 wale ulioungana nao kama marafiki wako maalum? 1 Je, hutapatwa na utungu kama mwanamke 2 aliye katika utungu wa kuzaa? 1
Jeremiah 25:32Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: 1 “Tazama! Maafa yanaenea 2 kutoka taifa moja hadi jingine; 1 tufani kubwa inainuka 2 kutoka miisho ya dunia.”
Jeremiah 50:43Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, 2 nayo mikono yake imelegea. 1 Uchungu umemshika, 2 maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 1