Mark 4:1
Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umekusanyika kumzunguka ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
2Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema:
Cross References
Matthew 13:1Siku iyo hiyo Yesu akatoka nje ya nyumba, akaketi kando ya bahari.
Mark 3:7Yesu pamoja na wanafunzi wake wakaondoka huko wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya ukamfuata.
Luke 8:4Umati mkubwa wa watu ulipokuwa ukija kwa Yesu kutoka kila mji, akawaambia mfano huu: