Mark 4:15
Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Job 1:6Siku moja wana wa Mungu + 1:6 Wana wa Mungu hapa ina maana malaika au viumbe vya mbinguni. walikwenda kujionyesha mbele za Bwana. Shetani + 1:6 Shetani hapa ina maana ya mshtaki wa watakatifu. naye akaja pamoja nao.
Zechariah 3:1Kisha akanionyesha Yoshua, + 3:1 Yoshua kwa Kiebrania ni Yeshua, maana yake ni Yehova ni wokovu. kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki.
Matthew 13:19Mtu yeyote anaposikia neno la Ufalme naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake. Hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia.
Mark 4:4Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila.
Luke 14:18“Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’
Acts 17:18Kisha baadhi ya Waepikureo na Wastoiko wenye falsafa wakakutana naye. Baadhi yao wakasema, “Je, huyu mpayukaji anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Inaonekana anasema habari za miungu ya kigeni.” Walisema haya kwa sababu Paulo alikuwa anahubiri habari njema kuhusu Yesu na ufufuo wa wafu.