Mathayo 1:16
naye Yakobo akamzaa Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo. + 1:16 Kristo maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And Jacob begat Joseph the husband of Mary, of whom was born Jesus, who is called Christ.
In Context
15Eliudi akamzaa Eleazari, 2 Eleazari akamzaa Matani, 2 Matani akamzaa Yakobo, 2
Cross References
Matthew 2:13Walipokwisha kwenda zao, malaika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto akamwambia, “Ondoka, mchukue mtoto na mama yake mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapowaambia, kwa maana Herode anataka kumtafuta huyu mtoto ili amuue.”
Matthew 27:22Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?” Wakajibu wote, “Msulubishe!”
Luke 1:27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria.
Luke 2:4Hivyo Yosefu akapanda kutoka mji wa Nazareti ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi.
Luke 2:10Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote.
Luke 3:23Yesu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yosefu, 1 Yosefu alikuwa mwana wa Eli, 1