Matthew 1:20
Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 46:3Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa.
Judges 13:3Malaika wa Bwana akamtokea huyo mwanamke na kumwambia, “Wewe ni tasa na huna mtoto, lakini utachukua mimba na utamzaa mtoto mwanaume.
1 Kings 17:13Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unitengenezee mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyo navyo kisha uniletee na ndipo utayarishe chochote kwa ajili yako na mwanao.
Job 33:15Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, 2 katika maono ya usiku, 1 wakati usingizi mzito uwaangukiapo 2 wanadamu wasinziapo vitandani mwao, 1
Psalms 94:19Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, 2 faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu. 1
Psalms 143:8Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, 2 kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. 1 Nionyeshe njia nitakayoiendea, 2 kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. 1