Matthew 1:21
Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu, + 1:21 Yesu ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua. Maana yake ni Yehova ni wokovu. kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
22Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema:
Cross References
Genesis 17:19Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki. + 17:19 Isaki maana yake Kucheka. Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake.
Genesis 18:10Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.
2 Kings 4:16Elisha akamwambia, “Mwaka ujao, wakati kama huu utabeba mwana mikononi mwako.” Yule mama akapinga, akasema, “La hasha, bwana wangu, usimpotoshe mtumishi wako, ee mtu wa Mungu!”
Isaiah 12:1Katika siku ile utasema: 1 “Nitakusifu wewe, Ee Bwana. 2 Ingawa ulinikasirikia, 1 hasira yako imegeukia mbali 2 nawe umenifariji. 1
Jeremiah 23:6Katika siku zake, Yuda ataokolewa 2 na Israeli ataishi salama. 1 Hili ndilo jina atakaloitwa: 2 Bwana Haki Yetu.
Ezekiel 36:25Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka uchafu wenu wote na kutoka sanamu zenu zote.