Mathayo 11:27
“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia. 1 Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
26Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.
28“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Cross References
Matthew 28:18Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
John 1:18Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha. 1 Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji (Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18)
John 5:21Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda.
John 7:29Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.”
John 13:3Yesu akijua ya kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka yake na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu,
John 17:2Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa.