Matthew 22:16
Wakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Yesu katika maneno yake.
17Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
Cross References
1 Kings 22:14Lakini Mikaya akasema, “Hakika kama Bwana aishivyo, nitamwambia kile tu Bwana atakachoniambia.”
Psalms 5:9Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, 2 mioyo yao imejaa maangamizi. 1 Koo lao ni kaburi lililo wazi, 2 kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu. 1
Psalms 55:21Mazungumzo yake ni laini kama siagi, 2 hata hivyo vita vimo moyoni mwake. 1 Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, 2 hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa. 1
Isaiah 59:13Uasi na udanganyifu dhidi ya Bwana, 2 kumgeuzia Mungu wetu kisogo, 1 tukichochea udhalimu na maasi, 2 tukinena uongo ambao mioyo yetu imeuhifadhi. 1
Ezekiel 33:30“Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule utokao kwa Bwana.’
Malachi 2:6Fundisho la kweli lilikuwa kinywani mwake, wala hakuna uongo wowote uliopatikana katika midomo yake. Alitembea nami katika amani na unyofu, naye akawageuza wengi kutoka dhambini.