Matthew 3:1
Siku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Uyahudi, akisema,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In those days came John the Baptist, preaching in the wilderness of Judaea,
In Context
2“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”
Cross References
Joshua 14:10“Sasa basi, kama vile Bwana alivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na mitano tangu wakati alipomwambia Mose jambo hili, wakati Waisraeli wakiwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo, nina umri wa miaka themanini na mitano!
Judges 1:16Wazao wa yule Mkeni, baba mkwe wa Mose, wakapanda pamoja na watu wa Yuda kutoka Mji wa Mitende, + 1:16 Yaani Yeriko. wakaenda kuishi miongoni mwa watu wa jangwa ya Yuda huko Negebu karibu na mji wa Aradi.
Matthew 3:8Basi zaeni matunda yastahiliyo toba.
Matthew 11:11Amin, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni ni mkuu kuliko Yohana.
Matthew 16:14Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.”
Matthew 21:25Ubatizo wa Yohana, ulitoka wapi? Je, ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’