Nehemia 2:19
Lakini Sanbalati Mhoroni, Tobia afisa Mwamoni, na Geshemu Mwarabu waliposikia kuhusu jambo hili, walitudhihaki na kutucheka. Wakauliza, “Ni nini hiki mnachokifanya? Je, mnaasi dhidi ya mfalme?”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Ezra 4:15ili kwamba ufanyike uchunguzi kwenye kumbukumbu ya maandishi ya waliokutangulia. Katika kumbukumbu hizi utagundua kwamba mji huu ni wa maasi, unaowataabisha wafalme na majimbo, ni mahali pa maasi tangu zamani. Ndiyo maana mji huu uliharibiwa.
Nehemiah 4:1Sanbalati aliposikia kwamba tulikuwa tunajenga ukuta upya, alikasirika na akawa na uchungu sana. Aliwadhihaki Wayahudi
Nehemiah 6:6iliyokuwa imeandikwa: “Habari imeenezwa miongoni mwa mataifa, naye Geshemu anasema kwamba ni kweli, kuwa wewe na Wayahudi mnafanya hila ya kuasi, ndiyo sababu mnajenga ukuta. Zaidi ya hayo, kufuatana na taarifa hizi, karibuni utakuwa mfalme wao,
Job 30:1“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, 1 watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau 2 kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. 1
Psalms 79:4Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu, 2 cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. 1
Psalms 80:7Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; 2 utuangazie uso wako, 2 nasi tuweze kuokolewa. 1