Numbers 12:13
Hivyo Mose akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And Moses cried unto the LORD, saying, Heal her now, O God, I beseech thee.
In Context
Cross References
Exodus 15:26Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, niwaponyaye.”
Numbers 14:2Waisraeli wote wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa!
Numbers 16:41Siku iliyofuata jumuiya yote ya Kiisraeli wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, wakisema, “Mmewaua watu wa Bwana.”
1 Samuel 12:23Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya Bwana kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka.
1 Kings 13:6Kisha mfalme akamwambia mtu wa Mungu, “Niombee kwa Bwana Mungu wako ili mkono wangu upate kupona.” Kwa hiyo mtu wa Mungu akamwombea kwa Bwana, nao mkono wa mfalme ukapona na kuwa kama ulivyokuwa hapo kwanza.
Jeremiah 17:14Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka; 2 uniokoe nami nitaokoka, 2 kwa maana wewe ndiwe ninayekusifu. 1