Numbers 12:14
Bwana akamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
13Hivyo Mose akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”
Cross References
Leviticus 13:45“Mtu mwenye ugonjwa kama huo wa kuambukiza ni lazima avae nguo zilizoraruka, awachilie nywele zake bila kuzichana, afunike sehemu ya chini ya uso wake, na apige kelele, ‘Najisi! Najisi!’
Numbers 5:2“Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu yeyote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao, + 5:2 Ugonjwa wa ngozi uambukizao hapa ina maana ya ukoma. au anayetokwa na majimaji ya aina yoyote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti.
2 Chronicles 26:20Azaria kuhani mkuu pamoja na makuhani wengine wote walipomtazama wakaona kwamba alikuwa na ukoma penye kipaji chake cha uso wakaharakisha kumtoa nje. Naam, hata yeye mwenyewe alikuwa anatamani kuondoka kwa sababu Bwana alikuwa amempiga.
Job 30:10Wananichukia sana na kujitenga nami, 2 wala hawasiti kunitemea mate usoni. 1
Matthew 26:67Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi