Numbers 19:16
“Mtu yeyote aliyeko nje mahali pa wazi agusaye mtu aliyeuawa kwa upanga au mtu aliyekufa kwa kifo cha kawaida, au mtu yeyote agusaye mfupa wa mtu aliyekufa au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15nacho kila chombo kisicho na kifuniko juu yake kitakuwa najisi.
Cross References
Leviticus 21:1Bwana akamwambia Mose, “Sema na makuhani, wana wa Aroni, uwaambie: ‘Kamwe kuhani asijitie unajisi kwa utaratibu wa kiibada kwa ajili ya mtu wake yeyote anayekufa,
Numbers 6:6Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili ya Bwana hatakaribia maiti.
Numbers 19:11“Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote atakuwa najisi kwa siku saba.
Ezekiel 39:11“ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki kuelekea baharini. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote ya wajeuri watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu. + 39:11 Hamon-Gogu maana yake Makundi ya wajeuri wa Gogu.
Ezekiel 39:16(Pia mji uitwao Hamona + 39:16 Hamona maana yake Kundi (la wajeuri). utakuwa humo.) Hivyo ndivyo watakavyoisafisha nchi.’
Matthew 23:27“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo yanapendeza kwa nje, lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu.