Numbers 22:31
Kisha Bwana akafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa Bwana amesimama barabarani akiwa ameufuta upanga wake. Balaamu akainama, akaanguka kifudifudi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 21:19Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.
Numbers 24:4ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu, 2 ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi, + 24:4 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania (pia 24:16). 2 ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka: 1
Joshua 5:13Basi wakati Yoshua alipokuwa karibu na Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi uliofutwa kwenye ala. Yoshua akamwendea na kumuuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?”
2 Kings 6:17Kisha Elisha akaomba, “Ee Bwana, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo Bwana akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya moto, yamemzunguka Elisha pande zote.
1 Chronicles 21:16Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa Bwana akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.
Luke 24:16lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue.