Numbers 33:53
Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 3:18Wakati huo nilikuamuru: “ Bwana Mungu wako amekupa nchi hii uimiliki. Lakini ni lazima wanaume wenu wote wenye uwezo, wakiwa wamejiandaa tayari kwa vita, wavuke ngʼambo wakiwatangulia ndugu zako Waisraeli.
Deuteronomy 32:8Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao, 2 alipogawanya wanadamu wote, 1 aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa 2 sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli. 1
Joshua 21:43Kwa hiyo Bwana akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo.
Psalms 24:1Dunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake, 2 ulimwengu, na wote waishio ndani yake, 1
Jeremiah 27:5Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa yeyote inipendezavyo.
Daniel 4:25Wewe utafukuzwa mbali na wanadamu, nawe utaishi pamoja na wanyama pori; utakula manyasi kama ngʼombe, na kuloana kwa umande wa mbinguni. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye.