Numbers 9:8
Mose akawajibu, “Ngojeni mpaka nitafute kile Bwana anachoagiza kuwahusu ninyi.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And Moses said unto them, Stand still, and I will hear what the LORD will command concerning you.
In Context
Cross References
Exodus 14:13Mose akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu Bwana atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena.
Leviticus 24:12Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao.
2 Chronicles 20:17Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovu Bwana atakaowapatia, enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, naye Bwana atakuwa pamoja nanyi.’ ”
Psalms 85:8Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; 2 anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: 2 lakini nao wasirudie upumbavu. 1
Ezekiel 2:7Wewe lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa wanasikiliza au hawasikilizi, kwa kuwa wao ni watu waasi.
John 7:17Mtu yeyote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe.