Revelation 21:3
Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:11Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia.
1 Kings 8:27“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
Isaiah 12:6Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni, 2 kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”
Jeremiah 32:38Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Ezekiel 43:7Akasema, “Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi na mahali pa kuweka nyayo za miguu yangu. Hapa ndipo nitakapoishi miongoni mwa Waisraeli milele. Kamwe nyumba ya Israeli hawatalinajisi tena Jina langu takatifu, yaani, wao wala wafalme wao, kwa ukahaba wao na kwa sanamu zao zisizokuwa na uhai za wafalme wao katika mahali pao pa juu pa kuabudia miungu.
Zechariah 13:9Hii theluthi moja nitaileta katika moto; 2 nitawasafisha kama fedha isafishwavyo 2 na kuwajaribu kama dhahabu. 1 Wataliitia Jina langu 2 nami nitawajibu; 1 nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ 2 nao watasema, ‘ Bwana ni Mungu wetu.’ ”