Romans 6:23
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord.
In Context
Cross References
Genesis 3:19Kwa jasho la uso wako 2 utakula chakula chako 1 hadi utakaporudi ardhini, 2 kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, 1 kwa kuwa wewe u mavumbi 2 na mavumbini wewe utarudi.”
Ezekiel 18:4Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. 1
Matthew 25:46“Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”
John 3:36Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”
John 5:24“Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani.
John 6:27Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.”