Titus 1:7
Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 10:9“Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa Agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Proverbs 15:18Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, 2 bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi. 1
Proverbs 31:4“Ee Lemueli, haifai wafalme, 2 haifai wafalme kunywa mvinyo, 2 haifai watawala kutamani sana kileo, 1
Isaiah 28:7Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo, 2 wanayumbayumba kwa sababu ya kileo: 1 Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo, 2 wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo; 1 wanapepesuka wanapoona maono, 2 wanajikwaa wanapotoa maamuzi. 1
Ezekiel 44:21Kuhani yeyote asinywe mvinyo aingiapo katika ukumbi wa ndani.
Luke 12:42Yesu akamjibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa?