Tito 1:8
Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
But a lover of hospitality, a lover of good men, sober, just, holy, temperate;
In Context
Cross References
1 Samuel 18:1Baada ya Daudi kumaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi, naye akampenda kama nafsi yake mwenyewe.
1 Kings 5:7Hiramu aliposikia ujumbe wa Solomoni, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Bwana leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima kutawala juu ya taifa hili kubwa.”
Amos 5:15Yachukieni maovu, yapendeni mema; 2 dumisheni haki mahakamani. 1 Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote 2 atawahurumia mabaki ya Yosefu.
1 Thessalonians 2:10Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini.
1 Timothy 4:12Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi.
2 Timothy 2:22Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.