Tito 3:5
alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
4Lakini wema na upendo wa Mungu Mwokozi wetu ulipofunuliwa,
6ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu,
Cross References
Job 15:14“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, 2 au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu? 1
Psalms 51:10Ee Mungu, uniumbie moyo safi, 2 uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. 1
Psalms 86:5Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, 2 umejaa upendo kwa wote wakuitao. 1
Psalms 130:7Ee Israeli, mtumaini Bwana, 2 maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, 2 na kwake kuna ukombozi kamili. 1
Isaiah 57:12Nitaifunua haki yako na matendo yako, 2 nayo hayatakufaidi. 1
Luke 1:50Rehema zake huwaendea wale wamchao, 2 kutoka kizazi hadi kizazi. 1