Zechariah 2:1
Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake!
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
I lifted up mine eyes again, and looked, and behold a man with a measuring line in his hand.
In Context
2Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?” Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”
Cross References
Isaiah 54:16“Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi, 2 yeye afukutaye makaa kuwa moto, 2 na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake. 1 Tena ni mimi niliyemwambia mharabu 2 kufanya uharibifu mwingi. 1
Ezekiel 40:3Akanipeleka huko, nami nikamwona mtu ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba. Alikuwa amesimama kwenye lango akiwa na kamba ya kitani na ufito wa kupimia mkononi mwake.
Ezekiel 47:4Akapima dhiraa 1,000 nyingine na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika magotini. Akapima dhiraa nyingine 1,000 na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kiunoni.
Zechariah 1:16“Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Revelation 11:1Ndipo nikapewa mwanzi uliokuwa kama ufito wa kupimia, nikaambiwa, “Nenda ukapime hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo.