Zechariah 3:4
Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
3Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika.
Cross References
1 Kings 22:19Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka upande wa kulia na wa kushoto.
Psalms 51:9Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, 2 na uufute uovu wangu wote. 1
Isaiah 6:5Ndipo nikalia, “Ole wangu! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi katikati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote.”
Isaiah 43:25“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako, 2 kwa ajili yangu mwenyewe, 2 wala sizikumbuki dhambi zako tena. 1
Isaiah 52:1Amka, amka, ee Sayuni, 2 jivike nguvu. 1 Vaa mavazi yako ya fahari, 2 ee Yerusalemu, mji mtakatifu. 1 Asiyetahiriwa na aliye najisi 2 hataingia kwako tena. 1
Isaiah 61:10Ninafurahia sana katika Bwana, 2 nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu. 1 Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu, 2 na kunipamba kwa joho la haki, 1 kama vile bwana arusi apambavyo 2 kichwa chake kama kuhani, 1 na kama bibi arusi ajipambavyo 2 kwa vito vyake vya thamani. 1