1 Nyakati 25:8
Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And they cast lots, ward against ward, as well the small as the great, the teacher as the scholar.
In Context
Cross References
Leviticus 16:8Aroni atapiga kura kwa ajili ya hao mbuzi wawili, mmoja kwa ajili ya Bwana na mwingine kwa ajili ya kubebeshwa dhambi. + 16:8 Yaani Azazeli , maana yake mbuzi wa ondoleo la dhambi ; pia ms. 10, 26.
1 Chronicles 15:22Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo.
1 Chronicles 24:31Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.
1 Chronicles 26:13Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.
2 Chronicles 23:13Athalia akaangalia, tazama alikuwepo mfalme akiwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta na waimbaji wakiwa na vyombo vya uimbaji, walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kupiga kelele, akisema, “Uhaini! Uhaini!”
Proverbs 16:33Kura hupigwa kwa siri, 2 lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.