1 Wafalme 1:39
Kuhani Sadoki akachukua pembe ya mafuta kutoka kwenye hema takatifu na kumtia Solomoni mafuta. Kisha wakapiga tarumbeta na watu wote wakapaza sauti wakisema, “Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 30:23“Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 500 + 30:23 Shekeli 500 ni sawa na kilo 6. za manemane ya maji, shekeli 250 + 30:23 Shekeli 250 ni sawa na kilo 3. za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri,
Exodus 30:35pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu.
1 Samuel 16:13Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama. 1 Daudi Katika Utumishi Kwa Sauli
1 Kings 1:34Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wamtie mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, ‘Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!’
2 Kings 9:13Wakaharakisha kuvua mavazi yao, na kuyatandaza chini ya Yehu ili akanyage juu kwenye ngazi ya nje. Kisha wakapiga tarumbeta na kupaza sauti wakisema, “Yehu ni mfalme!” 1 Yehu Anamuua Yoramu Na Ahazia
1 Chronicles 29:22Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Bwana siku ile. Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya Bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani.