Exodus 30:35
pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 28:41Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Leviticus 2:13Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya Agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote.
1 Kings 1:39Kuhani Sadoki akachukua pembe ya mafuta kutoka kwenye hema takatifu na kumtia Solomoni mafuta. Kisha wakapiga tarumbeta na watu wote wakapaza sauti wakisema, “Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!”
Psalms 133:2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, 2 yakitiririka kwenye ndevu, 1 yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, 2 mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. 1
Song of Solomon 1:3Manukato yako yananukia vizuri, 2 jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. 1 Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! 1
John 12:3Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja + 12:3 Painti moja ni kama nusu lita. yenye manukato ya nardo + 12:3 Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri. safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.