1 Wafalme 21:27
Ahabu aliposikia maneno haya, akararua nguo zake, akavaa nguo za gunia na kufunga. Akalala na kujifunika nguo za gunia na kwenda kwa unyenyekevu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
28Ndipo neno la Bwana lilipomjia Eliya Mtishbi kusema,
Cross References
Exodus 33:4Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote.
2 Samuel 12:16Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto. Akafunga na akaingia ndani ya nyumba yake akawa siku zote analala sakafuni usiku kucha.
2 Kings 18:37Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia yale jemadari wa jeshi aliyoyasema.
1 Chronicles 21:16Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa Bwana akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.
Isaiah 22:12Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 aliwaita siku ile 1 ili kulia na kuomboleza, 2 kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia. 1
Isaiah 58:5Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua, 2 siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza? 1 Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete, 2 na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu? 1 Je, huo ndio mnaouita mfungo, 2 siku iliyokubalika kwa Bwana? 1