2 Nyakati 10:16
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: 1 “Tuna fungu gani kwa Daudi? 2 Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. 1 Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli, 2 angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 20:27Lakini siku iliyofuata, siku ya pili ya mwezi, kiti cha Daudi kilikuwa wazi tena. Kisha Sauli akamwambia mwanawe Yonathani, “Kwa nini mwana wa Yese hajaja chakulani jana wala leo?”
1 Samuel 22:7Sauli akawaambia, “Sikilizeni enyi watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa ninyi nyote mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya ninyi nyote majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia?
1 Samuel 22:13Sauli akamwambia, “Kwa nini umepanga shauri baya dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, ukampa vyakula na upanga, tena hukumuuliza Mungu kwa ajili yake, na kwa sababu hiyo ameasi dhidi yangu na kunivizia, kama afanyavyo leo?”
2 Samuel 15:13Mjumbe akaja na kumwambia Daudi, “Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu.”
2 Samuel 20:1Basi, kulikuwa na mtu mbaya sana aliyeitwa Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini, aliyekuwako huko. Akapiga tarumbeta na kupaza sauti, 1 “Hatuna fungu katika Daudi, 2 wala hatuna sehemu 2 katika mwana wa Yese! 1 Kila mtu aende hemani mwake, 2 enyi Israeli!”
1 Kings 11:34“ ‘Lakini sitauondoa ufalme wote kutoka mikononi mwa Solomoni, nimemfanya mtawala siku zote za maisha yake kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, niliyemchagua na ambaye aliyatunza maagizo na amri zangu.