2 Samweli 20:1
Basi, kulikuwa na mtu mbaya sana aliyeitwa Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini, aliyekuwako huko. Akapiga tarumbeta na kupaza sauti, 1 “Hatuna fungu katika Daudi, 2 wala hatuna sehemu 2 katika mwana wa Yese! 1 Kila mtu aende hemani mwake, 2 enyi Israeli!”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 13:13kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu),
Judges 19:22Walipokuwa wakijiburudisha, watu waovu wa mji huo, wakaizingira ile nyumba. Wakagonga mlango na kusema na yule mzee mwenye nyumba, “Mtoe nje yule mtu aliyeingia kwako, tupate kumlawiti.”
1 Samuel 2:12Wana wa Eli walikuwa watu wabaya kabisa, hawakumheshimu Bwana.
1 Samuel 30:22Lakini watu wote waovu na wakorofi miongoni mwa wafuasi wa Daudi wakasema, “Kwa sababu hawakwenda pamoja nasi, hatutagawana nao nyara tulizorudisha. Lakini, kila mtu aweza kuchukua mkewe na watoto wake na kuondoka.”
2 Samuel 16:11Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, yeye ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuuondoa uhai wangu. Je, si zaidi sana kwa huyu Mbenyamini! Mwacheni, acha alaani, kwa maana Bwana amemwambia afanye hivyo.
2 Samuel 23:6Lakini watu waovu wote 2 watatupwa kando kama miiba, 2 ambayo haikusanywi kwa mkono. 1