2 Nyakati 15:6
Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And nation was destroyed of nation, and city of city: for God did vex them with all adversity.
In Context
Cross References
Judges 2:14Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
2 Chronicles 13:17Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli.
2 Chronicles 36:17Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza.
Isaiah 10:6Ninamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu, 2 ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha, 1 kukamata mateka na kunyakua nyara, 2 pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani. 1
Amos 3:6Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari, 2 watu hawatetemeki? 1 Mji upatwapo na maafa, 2 je, si Bwana amesababisha? 1
Matthew 24:7Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali.