2 Nyakati 20:26
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Beraka + 20:26 Bonde la Beraka maana yake Bonde la Kusifu. kwa maana huko ndiko walikomsifu Bwana. Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka mpaka leo.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 32:20Hakikisheni mmesema, ‘Mtumishi wako Yakobo anakuja nyuma yetu.’ ” Kwa kuwa alifikiri, “Nitaweza kumtuliza kwa zawadi hizi ninazotanguliza, hatimaye, nitakapomwona, huenda atanikubali.”
Exodus 17:15Mose akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi. + 17:15 Yehova Nisi maana yake ni Bwana ni Bendera yangu.
2 Samuel 22:1Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli.
Psalms 103:1Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. 2 Vyote vilivyomo ndani yangu 2 vilihimidi jina lake takatifu. 1
Isaiah 62:4Hawatakuita tena Aliyeachwa, 2 wala nchi yako kuiita Ukiwa. 1 Bali utaitwa Hefsiba, + 62:4 Hefsiba maana yake Yeye ninayemfurahia. 2 nayo nchi yako itaitwa Beula, + 62:4 Beula maana yake Aliyeolewa. 1 kwa maana Bwana atakufurahia, 2 nayo nchi yako itaolewa. 1
Acts 1:19Kila mtu Yerusalemu akasikia habari hizi, kwa hiyo wakapaita mahali hapo kwa lugha yao, Akeldama, yaani Shamba la Damu).