2 Chronicles 30:27
Ndipo makuhani na Walawi wakasimama wakawabariki watu, naye Mungu akawasikia, kwa sababu maombi yao yalifika mbinguni, makao yake matakatifu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Numbers 6:23“Mwambie Aroni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni: 1
Deuteronomy 26:15Angalia chini kutoka mbinguni, maskani yako matakatifu, uwabariki watu wako Israeli pamoja na nchi uliyotupa kama ulivyoahidi kwa kiapo kwa baba zetu, nchi inayotiririka maziwa na asali.” 1 Fuata Maagizo Ya Bwana
1 Kings 8:39basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote),
2 Chronicles 23:18Kisha Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la Bwana mikononi mwa makuhani, waliokuwa Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za Bwana kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, kwa kushangilia na kuimba kama Daudi alivyokuwa ameagiza.
Isaiah 57:15Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, 2 yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: 1 “Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu, 1 lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu 2 na mwenye roho ya unyenyekevu, 1 ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu 2 na kuihuisha mioyo yao waliotubu. 1
Isaiah 66:1Hili ndilo asemalo Bwana, 1 “Mbingu ni kiti changu cha enzi, 2 nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. 1 Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu? 2 Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi? 1