Isaya 57:15
Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, 2 yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: 1 “Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu, 1 lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu 2 na mwenye roho ya unyenyekevu, 1 ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu 2 na kuihuisha mioyo yao waliotubu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 15:11“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Bwana? 2 Ni nani kama Wewe: 3 uliyetukuka katika utakatifu, 3 utishaye katika utukufu, 3 ukitenda maajabu? 1
Exodus 40:34Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu.
Deuteronomy 33:27Mungu wa milele ni kimbilio lako, 2 na chini kuna mikono ya milele. 1 Atamfukuza adui yako mbele yako, 2 akisema, ‘Mwangamize yeye!’ 1
1 Kings 8:27“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
2 Chronicles 34:27Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Mungu uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu na uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema Bwana.
Job 22:29Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’ 2 ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo. 1