2 Kings 21:13
Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kamba ya kupimia iliyotumika dhidi ya Samaria, na timazi iliyotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu. Nitaifutilia mbali Yerusalemu kama mtu afutaye sahani, nikiifuta na kuifunikiza.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 21:21‘Nitaleta maafa juu yako. Nitaangamiza uzao wako na kukatilia mbali kutoka kwa Ahabu kila mzaliwa wa mwisho wa kiume katika Israeli, wa mtumwa au wa mtu huru.
2 Kings 10:11Hivyo Yehu akaua kila mtu huko Yezreeli aliyekuwa amebaki wa nyumba ya Ahabu, ikiwa ni pamoja na wakuu wake, rafiki zake wa karibu, na makuhani wake. Hakuacha yeyote anusurike.
Isaiah 10:22Ingawa watu wako, ee Israeli, ni wengi kama mchanga wa pwani, 2 ni mabaki yao tu watakaorudi. 1 Maangamizi yamekwisha amriwa, 2 ni mengi tena ni haki. 1
Isaiah 28:17Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia 2 na uadilifu kuwa timazi; 1 mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo, 2 nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha. 1
Jeremiah 25:9nitayaita mataifa yote ya kaskazini na mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli,” asema Bwana. “Nitawaleta waishambulie nchi hii na wakazi wake wote, na dhidi ya mataifa yote yanayowazunguka. Nitawaangamiza kabisa na kuwafanya kitu cha kuchukiwa na kudharauliwa, na kuwa magofu daima.
Ezekiel 23:31Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako.