2 Samweli 23:18
Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 2:18Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa.
2 Samuel 10:10Akawaweka waliobaki chini ya uongozi wa Abishai nduguye na kuwapanga dhidi ya Waamoni.
2 Samuel 18:2Daudi akatuma vikosi vya askari: theluthi moja ilikuwa chini ya amri ya Yoabu, theluthi ya pili chini ya Abishai mwana wa Seruya nduguye Yoabu, na theluthi ya tatu chini ya Itai, Mgiti. Mfalme akaviambia vikosi, “Hakika mimi mwenyewe nitakwenda pamoja nanyi.”
1 Chronicles 2:16Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.
Ecclesiastes 4:12Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa, 2 watu wawili wanaweza 2 kumkabili adui na kumshinda. 1 Kamba ya nyuzi tatu 2 haikatiki kwa urahisi. 1 Maendeleo Ni Ubatili