2 Samweli 3:27
Basi Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando ndani ya lango, kama vile kuzungumza naye faraghani. Ili kulipiza kisasi damu ya nduguye Asaheli, Yoabu akamchoma mkuki tumboni palepale, naye akafa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Numbers 35:19Mlipiza kisasi cha damu atamuua muuaji; wakati akikutana naye, atamuua.
2 Samuel 2:19Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata.
2 Samuel 20:9Yoabu akamwambia Amasa, “U hali gani, ndugu yangu?” Kisha Yoabu akamshika Amasa ndevu kwa mkono wake wa kuume ili ambusu.
1 Kings 2:5“Sasa wewe mwenyewe unafahamu lile Yoabu mwana wa Seruya alilonitendea, lile alilofanya kwa majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yetheri. Aliwaua, akimwaga damu yao wakati wa amani kama vile ni kwenye vita, tena akaipaka damu ile kwenye mkanda uliokuwa kiunoni mwake na viatu alivyovaa miguuni mwake.
1 Chronicles 27:21kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria; 1 kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri; 1
Jeremiah 41:2Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga, wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi.